Vigezo na Masharti ya Faragha na Usalama wa Data

Tarehe ya mwisho kusasishwa: Julai 2026

Karibu kwenye Aziry Tech WhatsApp AI Sales Agent (SaaS). Tunachukulia faragha na usalama wa data zako kwa kiwango cha juu zaidi. Mfumo wetu umejengwa kwa misingi imara ya kiusalama kuhakikisha wewe na wateja wako mnakuwa na amani. Kwa kutumia huduma hii, unakubaliana na masharti yafuatayo:

1. Ulinzi wa Hali ya Juu & Usiri wa Ujumbe (End-to-End Authentication)

Ujumbe Wako ni Wako Tu. Mfumo huu unatumia mfumo wa usimbaji fiche (encryption) unaohakikisha kwamba hakuna mtu yeyote yule, hata sisi watengenezaji (Aziry Tech), anayeweza kusoma meseji zako na wateja wako. Ujumbe unaingia moja kwa moja kwenye server salama ukiwa umefichwa (encrypted) na kusomwa pekee na wewe (mmiliki halali) na AI inayokuhudumia ukiwa umeruhusu.

2. Umiliki na Udhibiti Kamili wa Data (Data Ownership)

Wewe ndiye mmiliki halali asilimia mia moja (100%) wa namba za simu, mawasiliano, na data zote za wateja wako. Mfumo wetu ni daraja tu la kurahisisha mawasiliano. Data zako hazitauzwa, hazitasambazwa, wala kutumiwa na mtu mwingine au kampuni nyingine yoyote nje ya makubaliano haya. Ukiamua kufuta akaunti yako, data zote zitafutwa moja kwa moja kwenye server zetu bila kubakiza nakala yoyote.

3. Haki ya Mteja Kuchagua (Ethical AI & Consent)

Kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, Mteja wako anapotuma ujumbe, atapewa uhuru wa kuchagua kuhudumiwa na AI au kuongea na wewe moja kwa moja. Hii inajenga uaminifu na uwazi. Endapo mteja atachagua kuongea na wewe (Rafiki), AI yetu itajizima kiotomatiki kwa mteja huyo.

4. Hifadhi na Ufutaji Kiotomatiki (Auto-Purge)

5. Wajibu Wako kama Mfanyabiashara

Unakubali kwamba:

5. Mabadiliko ya Masharti

Tunaweza kusasisha masharti haya mara kwa mara ili kuboresha usalama. Tutaweka taarifa hapa yakitokea mabadiliko makubwa.

← Rudi Kujisajili